Fabregas (jezi namba 10) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli
Pashapasha kuelekea mechi za kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya, Euro 2016. timu ya taifa ya Hispania jana imeichapa 2-1 Costa Rica katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.

Mapema dakika ya 6' Johan Venegas aliifungia Costa Rica bao la kuongoza, lakini dakika mbili baadaye Paco Alcacer akaisawazishia Hispania.

Dakika ya 30' Cesc Fabregas alifunga goli la pili na la ushindi kwa Hispania.
Febregas aliyekuwa nyota wa mchezo huo kwani licha ya kufunga, ndiye aliyemtengenezea Alcacer goli la kusawazisha.
0 comments:
Post a Comment