Chelsea wameripotiwa kukamilisha usajili wa kwanza majira ya kiangazi mwaka huu wakiinasa saini ya mlinzi wa miaka 17, raia wa Romania, Cristian Manea.
Mkurugenzi mkuu wa FC Viitorul Constanța amethibitisha usajili huo leo asubuhi kupitia vyombo vya habari kama inavyoonekana chini;
Breaking: Viitorul's CEO confirmed Manea's move to Chelsea and Ianis Hagi's leave for Fiorentina! #CFC
Imeelezwa kwamba, mlinzi huyo wa kulia atapelekwa kwa mkopo katika klabu ya Vitesse kwa msimu wa 2015/2016.
Kijana huyo mdogo wa Romania anakuwa miongoni mwa vijana wadogo waliojiunga na Chelsea, ingawa haingii kwenye kikosi cha kwanza.
Tazama video inayoonesha ufundi wa kijana huyu....
0 comments:
Post a Comment