Brazil wameshinda goli 1-0 dhidi ya Honduras mjini Porto Alegre ikiwa ni mechi ya kirafiki kujiandaa na michuano ya Copa America inayoanza kutimua vumbi leo ambapo wenyeji Chile wanafungua dimba na Ecuador majira ya saa nane na nusu usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Goli pekee la Brazil katika mechi hiyo ya jana lilifungwa dakika ya 33 ambapo mlinzi wa kulia wa Chelsea, Filipe Luis aliambaa na mpira winga ya kushoto na kupiga pasi murua ya mwisho kwa Roberto Firmino.
Filipe Luis hawakuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Chelsea msimu wa 2014/2015 na amekuwa akihusishwa kujiunga na Atletico Madrid majira ya kiangazi mwaka huu.
Brazil ambayo imeshinda mechi zote ilizocheza chini ya Dunga aliyeanza kufundisha baada ya kombe la dunia mwaka jana, watacheza mechi yao ya ufunguzi ya Copa America siku ya jumapili dhidi Peru.
Tazama video hii hapa chini ikionesha Pasi ya mwisho aliyopiga Filipe Luis, goli na highlights za mechi hiyo
0 comments:
Post a Comment