Monday, June 22, 2015

Brazil kwa matakwa yao wenyewe, wameamua kuendelea kushiriki michuano ya mataifa America ya Kusini (Copa America) bila ya huduma ya nahodha na mshambuliaji wa timu hiyo Neymar, mara baada ya kuamua kutoikatia rufaa adhabu ya kufungiwa mechi nne kwa mchezaji huyo aliyoipata katika mchezo dhidi ya Colombia.
Neymar alipewa adhabu hiyo Ijumaa kutokana na utovu wa nidhamu aliounesha baada ya timu yake kupoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Colombia Jumatano, wakati alipopewa kadi nyekundu baada ya kujaribu kumpiga kichwa Jeison Murill kabla ya kumtolea lugha chafu mwamuzi wa mchezo huo Enrique Osses.
Licha ya kukingiwa kifua na wachezaji wenzake dhidi ya tukio hilo la kipuuzi, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Brazil (CBF), limeamua kuachana na mapngo wao wa kuipinga adhabu hiyo ambayo, inamfanya akose michezo yote iliyobaki katika mashindano hayo.
"Baada ya kikao cha Jumapili kati ya Neymar na benchi zima la ufundi, imeamuriwa kwamba CBF limekubaliana na adhabu aliyopewa Neymar ya kufungiwa michezo minne na hivyo kukosa mechi zote zilizobaki katika michauno hii ya Copa America," taarifa ilieleza.
"Kwa pamoja timu na mchezaji wanaamini kuwa sheria iliyotumika kutoa hukumu dhidi ya kitendo hiki itendelea kutumika katika mashindano yote yanayoendeshwa na kusimamiwa na Shirikisho hili. Kwa kumalizia, benchi la ufundi la Brazil linaomba radhi kwa kumkosa mchezaji mwingine muhimu kabisa katika michuano hii.
"Neymar ataondoka Jumatatu (leo), kurejea nchini Brazil na kuiacha timu yake ambayo ipo katika hoteli ya Sheraton iliyopo Santiago kwa ajili ya maandalizi ya michezo inayofuata."
Brazil, ambao ni mabingwa mara tano wa kombe la dunia wamefuzu hatua ya robo fainali kutoka kundi Group C jana, baada ya kuichakaza Venezuela 2-1 katika dimba la Santiago.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video