Tovuti moja ya Romania leo imeripoti kwamba Arsenal imekamilisha usajili wa kinda wa miaka 16, raia wa Romania, Vlad Dragomir.
Picha inayoonesha Dragomir akiwa na jezi ya Arsenal baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na miamba hiyo ya ligi kuu England imesambaa leo kwenye mitandao.
Dragomir ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Vijana ya Romania wenye umri chini ya miaka 16 anacheza safu ya kiungo, sehemu ya kulia au kushoto na atatambulishwa Juni 29 mwaka huu.
Arsenal watailipa klabu ya ACS Poli Timisoara kiasi fedha kinachokadriwa kuwa Euro laki moja.
Hapa chini ni video inayoonesha Highlights za Dragomir;
0 comments:
Post a Comment