Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Ombi la Yanga linakwenda kinyume cha Azimio la Bagamoyo la 2007' linalotaka timu za VPL ziwe na wachezaji wa kigeni wasiozidi watatu.'
SIKU chache baada ya kung'olewa katika michuano ya kimataifa, uongozi wa Yanga umeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuruhusu klabu za Ligi Kuu kusajili wachezaji wengi wa kigeni.
Yanga, mabingwa mara 25 wa Tanzania Bara, Jumamosi waling'olewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 ugenini dhidi ya timu iliyosheheni wachezaji nyota na walioshiba ya Etoile Sportive du Sahel (ESS) kwenyhe Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia.
Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, ameweka wazi kwamba kuwapo kwa kanuni inayozuia klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kuwa na nyota zaidi ya watano wa kigeni, kumechangia timu kutofanya vyema dhidi ya ESS.
"Timu yetu ilicheza vizuri Tunisia, tunaamini Waarabu hawatafurahia kupangwa na Yanga tena. Tunaomba TFF waruhusu timu zisajili wachezaji wengi wa kigeni ikiwezekana nane ili ziwe na uwezo mkubwa wa kupambana katika michuano ya kimataifa," amesema Muro.
Ombi la Yanga linakwenda kinyume cha Azimio la Bagamoyo la 2007 linalotaka klabu za Ligi Kuu nchini kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watatu. Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2014 zinaruhusu klabu za VPL kuwa na wachezaji wa kigeni wasiozidi watano.
Kwa muda mrefu Yanga na timu za Tanzania kwa ujumla zimekuwa zikinyanyasika kwa kutolewa katika michuano ya Afrika pindi zinapokutana na timu kutoka Kaskazini mwa Afrika huku Wanajangwani wakiwa ni wateja wa kutupwa kwa timu hizo.
Rekodi inaonyesha tangu Yanga ianze kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), haijawahi kuitoa timu kutoka Afrika ya Kaskazini.
Katika miaka mitano iliyopita safari ya Yanga ilifia Misri, Libya na Tunisia. 2008 Yanga ilimaliza nafasi ya pili VPL na kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho na ilitolewa dhidi Al-Akhdar ya Libya kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0 baada ya kutoka suluhu Libya kisha kufungwa 1-0 kweenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
2009 Yanga ilinyakua ubingwa wa VPL na kushiriki Klabu Bingwa Afrika, lakini ikang'olewa kwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya Esparence ya Tunisia.

Yanga ilifungwa 3-0 Tunisia.
2011 Yanga ikashiriki tena michuano hiyo, lakini ikatupwa nje kwa kipigo cha jumla ya 3-1 dhidi ya Al Ahly ya Misri (sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam katika mechi ya pili).
Msimu wa 2012/13 Wanajangwani wakashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, lakini safari yao ikaishia mikononi mwa Zamelak ya Misri wakitoka sare ya 1-1 Dar es Salaam kabla ya Yanga kudundwa 1-0 jijini Cairo.
Mwaka jana Yanga licha ya kuanza vyema kwa kuwatoa Wacomoro, Komorozine kwa jumla ya mabao 12-2, wakang'olewa Al Ahly kwa matuta 6-5 baada ya sare ya 1-1 (Yanga walioshinda 1-0 Dar es Saaam huku Al Ahly nao wakishinda 1-0 nchini Misri).

0 comments:
Post a Comment