Wednesday, May 6, 2015

Na. Richard Bakana, Dar es salaam
Mabingwa wapya wa ligi kuu ya Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans leo wamekabidhiwa kikombe chao cha ubingwa baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC ambao ndio walikuwa watetezi ambapo mtanange huo ulimalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Andrey Coutinho kwa free Kick ambayo iliingia langoni moja kwa moja kunako dakika ya 12 kipindi cha kwanza lakini goli hilo halikudumu kwa muda mrefu kwani Bryson Raphael aliweza kusawazisha na kufanya timu hizo zinaenda mapumziko zikiwa 1-1.

Huku mvua kubwa ikinyesha mwanzo mwisho Azam FC walijihakikishia nafasi ya kushiriki Michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kwa kuwa katika nafasi ya pili baada Agrey Morris kufunga bao la pili katika dakika ya 33 ya kipindi cha pili na kufanya matokeo yawe 2-1.

Katika sherehe hizo za kukabidhiwa Kombe hilo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenela Mkangala yeye ndio alikuwa mgeni rasmi ambapo aliwavisha medari mabingwa hao pamoja na kuwakabidhi kikombe chao huku Azam FC wao wakivishwa Medari tu.

ILIKUA HIVI DAKIKA 45 ZA MWANZO

Dakiakya 2 azam wanapata kona ya kwanza lakini wanashindwa kuifanyia kazi
Tambwe anaikosesha bao Yanga dakika ya 3 baada ya kuingiza krosi ambayo inakosa macho na kuokolewa na mabeki wa Azam.

Azam wanakosa bao baada ya Brian Majwega kupiga krosi lakini Tchetche anachelewa na kuokolewa na mabrki wa Yanga ikiwa ni dakika ya 6.

Dakia ya 7 Azam FC wanakosa bao baada ya Kipre Tchetche kupaisha mpira juu akiwa na kipa baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Himid Mao.

Dakika ya 12 Yanga wanapata bao la kwanza baada ya Andry Coutinho kupiga mpira wa Adhabu na kuingia moja kwa moja .

Dakika ya 14 Azam wanasawazisha bao kupitia kwa Bryson Raphael baada ya Mwaikimba kukosa bao akiwa pekee yeye na mpira.

Dany Mrwanda anakosa bao kunako dakika ya 21 baada ya kupiga shuti kali na kutoka nje kidogo ya lango la Azam FC.

Dakika ya 27 Yanga wanapata faulo baada ya Shomari Kapombe kumfanyia madhambi Coutinho ambapo mpira ulipigwa na kuishia kwa mabeki wa Azam ,

Azam FC wanakosa bao katika dakika ya 28 baada ya Kipre Tchetche kupiga shuti ambalo lilimbabatiza Deogratius Munishi Dida na kutoka nje.

Kipre Tchetche anakosa bao baada ya kupiga krosi ambayo mpira uligonga mwamba wa juu na kurudi Ndani ikiwa ni dakika ya 34.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Azam FC wanapata bao la pili dakika ya 33 kupitia kwa Agrey Morris.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video