MABINGWA wapya wa Tanzania Dar Young Africans kesho
wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mechi ya kesho kutwa ya ligi kuu soka
Tanzania bara dhidi ya Azam fc itayopigwa uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Yanga imewasili nchini majira ya saa tisa alasiri leo na
wachezaji wamepewa mapumziko kidogo na kesho wanarejea mzigoni.
Mkuu wa Idara ya habari na Masiliano wa Yanga, Jerry Muro
amesema kuna taarifa zinaenea kuwa Yanga wataibeba Azam ili ishike nafasi ya
pili, lakini wao kama Yanga hawana mpango huo, kila mtu atavuna alichopanda.
“Kesho tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari makao
makuu ya klabu kutolea ufafanuzi kwa kirefu kuhusu taarifa za sisi kuibeba
Azam, Yanga hatuwezi kufanya hivyo, kila mtu atavuna alichopanda, kama ulipanda
mchicha basi utavuna mchicha”. Amesema Muro.
0 comments:
Post a Comment