![]() |
Pluijm |
SIKU chache baada ya aliyekuwa winga wa Mbeya City, Deus
Kaseke kusajiliwa na Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der
Pluijm, amefunguka kuwa, anafurahi kumpata mchezaji huyo kwa kuwa aliacha
mapendekezo asajiliwe.
Winga huyo amepewa mkataba wa miaka miwili
mara tu baada ya kumaliza mkataba na timu ya awali ambayo ameitumikia kwenye
ligi kuu kwa misimu miwili tangu ilipopanda daraja 2013/14.
Akizungumza kutoka nchini Ghana, kocha huyo alisema
kuwa kwa sasa yupo mapumzikoni na familia yake lakini anafurahi kwa kuwa
alichopendekeza kimefanyiwa kazi.
Kocha huyo aliyeipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara,
alisema kuwa atarejea mapema nchini na hapo ndipo atapata nafasi ya kuzungumzia
zaidi masuala ya usajili.
“Siwezi kuzungumza sana, kwa sasa niko mapumzikoni lakini
ukweli ni kwamba alikuwa ni mmoja wa wachezaji niliokuwa nawahitaji kwenye
kikosi changu na nilimpendekeza katika ripoti yangu, mengi zaidi tutazungumza
nitakaporejea nchini mwezi Juni,” Pluijm aliiambia Salehjembe.
Winga huyo mwenye kasi na aliyefanikiwa kuichezea Mbeya City
kwa mafanikio makubwa licha ya msimu uliomalizika timu yake kuonekana kusuasua,
aliziingiza vitani klabu za Simba na Yanga zote zikiwania saini yake.
0 comments:
Post a Comment