MPAMBANO mkali wa masumbwi utafanyika Bagamoyo Mei 16 katika ukumbi wa che kwa che uliopo Bagamoyo mjini mpambano uho utawakutanisha bondia Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo atakaezipiga na Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam.
Mpambano uho utachezwa baada ya kila bondia kujigamba kuwa yeye ni zaidi ya mwenzie siku hiyo pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali wenye upinzani mkali katika masumbwi.
Rashidi Haruna atakumbana na Kaminja Ramadhani na Harid Hongo atakabiliana na Kishoki Mbishi mpambano mwingine ni Abdallah Samata atakaye zidunda na Maono Alli.
Mipambano hiyo inaletwa kwenu na Sharif Promotion wakati mgeni rasmi siku hiyo ni bondia kutoka morogoro Cosmas Cheka ambaye atakuja kuwapa nasaa mbalimbali mabondia na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuweza kusonga mbele kwa mchezo uho mjini Bagamoyo.
Kingilia katika mpambano uho ni Tsh, 8000 kwa V.I.P na kwaida ni sh. 5000.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na upatikanaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile.


0 comments:
Post a Comment