Mlinda mlango wa Bayern Munich Manuel Neuer amesisitiza kuwa ana hamu ya kumuonesha nyota wa Barcelona Messi, kwamba nani ni zaidi ya mwenzake wakati wawili hao wakikutana leo katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya hatua ya nusu fainali.
Neuer na Messi watakutana leo katika uwanja wa Nou Camp kwa mara ya kwanza kabisa tangu tangu wawili hao wakutane katika mchezo wa fainali ya kombe la dunia, ambapo Ujerumani waliifunga Argentina kwa bao 1-0.
Katika mchezo huo Neuer aliibuka mbabe mbele ya Messi huku leo pia akiamini kumficha makwapani kwa mara nyingine tena.
Manuel Neuer na Messi wakiwa wameshika zawadi zao baada ya mchezo wa fainali wa kombe la dunia nchini Brazil.
'Nina muheshimu sana Messi na pia nina heshima kubwa kwa vyote alivyofanya, ni mtu poa sana,' Neuer aliliambia L'Equipe.
'Lakini ni muhimu sana kuonesha mamlaka wakati tukiwa uwanjani na kuthibitisha nani ni zaidi ya mwenzake. Nilifanya hivyo katika kombe la dunia na nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
'Wote tuna dhumuni moja leo usiku. Ni muhmu sana kuonesha nafasi ya kutawala ili kujitengenezea heshima.
'Tunatakiwa tuitumia vizuri fursa ya kuwa na faida ya miili mikubwa, nidhamu na ari ya ushindi na ukatili pia.'
Ikumbukwe tu miaka miwili iliyopita, Bayern waliwatoa Barca kwa tofauti ta magoli 7-0.

0 comments:
Post a Comment