Baada ya kuukimbia uwanja wa CCM Kirumba kama uwanja wake
wa nyumbani kufuatia vichapo mfululizo Kagera sugar sasa kurejea Mwanza.
Hayo yamewekwa bayana na meneja wa wakata miwa hao Mohammedi Hussein alipokuwa akiteta na Mpenja blog.
Mohammedi Hussein amesema, kwa mujibu
wa ratiba, mchezo huo inaonesha utapigwa Mwanza na wao hawana sababu
ya kuukataa uwanja huo.
"Ni kweli tutamalizia mchezo wetu hapa mwanza ambapo
tumepiga kambi na ratiba inatuonesha tutacheza hapa, sisi hatuwezi
kuhamisha mchezo kupeleka uwanja mwingine kwa kuwa itakuwa gharama
kubwa"Alisema meneja huyo.
Mohammedi aliongeza kuwa kwa sasa timu hiyo haina cha
kupoteza kwa kuwa ligi yenyewe imefika mwisho ni bora wakubaliane na
matakwa ya bodi ya ligi ili wakajipange kwa msimu ujao.
"Ligi yenyewe imefika mwisho hatuna haja ya kuvutana na
bodi ya ligi wala TFF, kikubwa tunamaliza mchezo wetu na tunaenda kujipanga
kwa msimu ujao".Alisema.
Pia aliwaomba watu wa Mwanza kujitokeza kuishangilia timu
hiyo itakapo kuwa ikimaliza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Tanzania
prisons kwenye dimba la CCM Kirumba.
Ikumbukwe Kagera iliuchagua uwanja CCM Kirumba kama uwanja
wake wa nyumbani baada ya uwanja wa kaitaba kuwa katika marekebisho
lakini kufuatia kupoteza michezo mitatu mfululizo dhidi ya Mbeya city,
Azam fc pamoja na Ndanda timu hiyo iliamua kutimkia uwanja wa Kambarage
mkoani Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment