
Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO mkali wa masumbwi utafanyika
Bagamoyo Mei 16 katika ukumbi wa che kwa che uliopo Bagamoyo mjini,
mpambano huo utawakutanisha bondia Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo
atakaezipiga na Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam.
Mpambano huo utachezwa baada ya kila
bondia kujigamba kuwa yeye ni zaidi ya mwenzie, siku hiyo pia kutakuwa na
mapambano ya utangulizi yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali wenye
upinzani mkali katika masumbwi,
Rashidi Haruna atakumbana na Kaminja
Ramadhani na Harid Hongo atakabiliana na Kishoki Mbishi, mpambano
mwingine ni Abdallah Samata atakaye zidunda na Maono Alli
Mipambano hiyo inaletwa kwenu na
Sharif Promotion wakati mgeni rasmi siku hiyo ni bondia kutoka Morogoro
Cosmas Cheka, ambaye atakuja kuwapa nasaha mbalimbali mabondia na
mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuweza kusonga mbele kwa mchezo huo mjini Bagamoyo,
kingilia katika mpambano huo ni Tsh, 8000 kwa V.I.P na kwaida ni sh. 5000.
Katika mpambano wa siku hiyo, kutakuwa
na upatikanaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar vs Manny
Pacquaio 2015 , Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex
Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo
vitakavyokuwa vikigawiwa na kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia
watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa gharama nafuu na
kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi nchini.

0 comments:
Post a Comment