Kutoka katika jarida la Daily Telegraph linaripoti kwamba
mshambuliaji tokea klabu bingwa mtetezi ligi kuu ya Hispania Atletico
Madrid Antoine Greezman tayari ameshafungua milango ya kwenda Chelsea.
Nyota huyo huyo kwa mujibu wa klabu yake wanamtaka kuongeza
mkataba lakini yeye bado anasubiri kusikia Chelsea watasema nini hapo
baadae.
Kwa upande mwingine pia wakala wa mchezaji Angel Dimaria
kutoka Manchester united George Mendez amesema kwamba yupo katika
mazungumzo na klabu ya PSG ili wamnyakue nyota huyo.
Wakala huyo alikutana na timu hiyo mara ya mwisho wakati
PSG walipokutana na Fc. Barcelona katika mchezo wa ligi ya mabingwa
Ulaya mnamo mwezi wa 4 mwaka huu. Gazeti la Daily Express linaripoti.
Daily Mail nao wanaripoti kuwa Luis Enrique yuko katika
katika mipango ya kuondoka Fc. Barcelona hata kama akishinda Kombe la
ligi mwaka huu.
Enrique (45) hadi sasa ananyemelewa mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza Manchester City.
Nayo klabu ya Juventus imekataa tenda ya kitika cha paund
mil 80 ilimchukue nyota wake mdogo Paul Pogba itakapofika mnamo mwaka
kesho January 2016 na badala yake wanahitaji pesa zaidi kwani iliyotajwa
no ndogo, jarida la Tuttosport linaripoti.
Gareth Bale anaweza kuifanya Manchester United kutumia
kitita cha Paund mil 275 kufuatia usajili mwingine wa Memphis Depay
katika msimu huu wa majira joto.
Jarida la Daily Express linaripoti uwezekano mkubwa upo wa
Bale kujiunga na United haswa kutokana na msimu huu kutokuwa mzuri akiwa
na Real Madrid.


0 comments:
Post a Comment