Floyd Mayweather amempachika jina Manny Pacquiao na kumwita muoga na akatupilia mbali hoja ya pambano la marudiano dhidi ya bondia huyo raia wa Ufilipino.
Mayweather alishinda pambano hilo na kujikusanyia kitita cha dola za kimarekani milioni 300 katika pambano hilo ambalo lilipachikwa kina la pambano la Karne lililopigwa huko Las Vegas wikiendi iliyopita.
Pacquiao baadaye alidai kuwa, kabla ya pambano hilo alikuwa na jeraha la bega na hivyo kufanyiwa upasuaji siku ya jumatano wiki hii.
Manny Pacquiao alifichua jeraha lake la bega baada ya pambano dhidi ya Floyd Mayweather

Pacquiao aliweka picha yake baada ya kufanikisha zoezi la upasuaji wa bega katika akaunti yake rasmi ya Instagram

Baada ya pambano dhidi ya Pacquiao, Mayweather alionekana kusherehekea pamoja na mwanamuziki Chris Brown katika siku yake ya kuzaliwa.

Mayweather alipigwa picha akistarehe huko Las Vegas.




Akiafanyiwa mahojiano na kituo kimojawapo cha utangazaji nchini humo siku ya Jumamosi, alisema: 'visingizio, visingizio, visingizio.
'Alikuwa yuko haraka sana. mkono wake wa kushoto ulikuwa mwepesi mno. Vivyo hivyo kwa mkono wake wa kulia na alikuwa akiirusha yote kwa pamoja haraka sana na kwa nguvu.
'Mimi siwezi kuendekeza ujinga na na sitaki tena hadhira kuusikiliza ujinga huu Alipoteza. Anajua alipoteza. Nimemshusha thamani yote baada ya hili pambano.'
Baada ya pambano lile, Mayweather alimtumia sms mtangazaji wa ESPN na kumwambia angejiandaa kumpa ofa Pacquiao kwa ajili ya pambano lingine wakati atakapopona jeraha lake.
Lakini sasa amebadilisha maamuzi yake na sasa analiangalia pambano la mwezi Septemba, ambalo litakuwa ni pambano lake la 49.
'Nilimtumia ujumbe Stephen A Smith na kusema nitapambana naye tena? Ndio, lakini nimebadili maamuzi yangu,' Mayweather aliongeza.
'Kwa muda huu, hapana, kwa sababu anasingizia jeraha ndio sababu ya kupoteza, muoga. Kama ukipoteza we kubali tu kuwa umepoteza na useme kuwa, 'Mayweather, ulikuwa zaidi yangu'.'





0 comments:
Post a Comment