AFISA habari machachari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amewapongeza Dar Young Africans kwa kucheza vizuri licha ya kutolewa na Etoile du Sahel kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1 katika mechi mbili za hatua ya 16 bora ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Mechi ya kwanza Dar es salaam, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na jana Yanga wamefungwa 1-0 mjini Sousse, Tunisia.
Masau amendika kwenye ukurasa wake wa facebook: "Naipongeza kwa moyo wa dhati timu ya Yanga Sc ya Dar es salaam kwa hatua waliyofikia katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Pamoja na kutolewa, hakika vijana wamepambana, wameonesha uwezo, wamekufa kiume!
Kwakua mwakani mtashiriki tena Klabu Bingwa, jipangeni mapema ili mfanye vizuri zaidi na kuiletea heshima Tanzania katika medani hii ya soka.
Sisi Ruvu Shooting msimu huu wa ligi VPL hatujafanya vizuri sana lakini tuna malengo makubwa ya kuleta mabadiliko makubwa ya soka la nchi yetu. Tunadhani siku za karibuni tutatawazwa kuwa mabingwa wa soka nchini na tutaiwakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa kwa ukamilifu na mafanikio makubwa kwani, uwezo tunao!
Nyie mnaoshiriki mashindano ya Kimataifa sasa, tusafishieni njia kwa kufanya vizuri japo kwa asilimia fulani ili sisi Wanaume tutakapopata nafasi hiyo tuiondoe Tanzania katika aibu ya kuonekana hatuna uwezo Kimataifa, Kisoka.
Yanga Sc, "big up", mmekufa kiume!
0 comments:
Post a Comment