Sunday, May 3, 2015

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesisitiza kuwa hapendi utaratibu wa timu kupigiwa makofi na timu pinzani huku wachezaji wa timu pinzani wakiwa wamejipanga mstari kuashiria heshima kwa mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Uingereza.
Mourinho amesema kuwa asingependa timu yake kufanyiwa hivyo na Liverpool endapo watatwaa ndoo ya ligi kuu nchini Uingereza kwa kuwafunga Crystal Palace.
Lakini kwa upande wake kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa wao hawana tatizo juu ya hilo na watafanya hivyo kama utaratibu unavyoelekeza pale watakapovaana na Chelsea katika uwanja wa  Stamford Bridge wiki ijayo.
Mourinho, ameendelea kusema kuwa utaratibu huo ni kama unalazimisha timu nyingine kutoa heshima ya lazima pasipo ridhaa yao.
"Mimi sipendi kabisa huu utaratibu," aliwaambia waandishi. "Nadhani Uhispania walifanya kwetu sisi wakati niko Real Madrid.
"Kama ni utaratibu basi sawa sina tatizo na hilo, lakini unaweza kuonesha heshima kwa bingwa husika kwa njia mbadala.
"Kama baadhi yao unakuta hawataki kuwa hapo ila wapo hapo kwa sababu wameambiwa wawepo, mi naona si vyema, kizuri ni maridhiano tu."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video