Tuesday, May 12, 2015

Sergio Aguero amefichua kwamba maelekezo aliyoyapata kutoka kwa daktari lishe wa Lionel Messi yamemfanya aimarike kwa kiasi kikubwa katika ubora wake pindi awapo uwanjani akiitumikia klabu yake ya Manchester City.
Mshambuliaji huyo raia wa Argentina, mpaka sasa ameshafunga mabao 31 katika mashindano yote msimu huu, huku akitoa mchango mkubwa sana kwa safu ya ushambuliaji wa timu hiyo licha ya msimu mbovu kwa timu yake.
Mwaka jana, Messi ambaye ni raia mwenza wa Arguero alimuelekeza aende kwa Giuliano Poser, ambaye ni mtaalamu wa masula ya lishe huko nchini Italy na hali hiyo Arguero amesema imemsaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza majeraha ya mara kwa mara ambayo yalikuwa yakimsumbua sana katika msimu wa 2013-14
Arguero alisema: “Ni vitu vingi sana ambavyo nilitakiwa kubadilisha, hasa chakula ili niishi maisha yenye afya nzuri.
“Sijapata majeraha yoyote ya misuli tangu msimu uanze, ni jeraha la goti pekee ambalo  limenisumbua msimu huu.
“Wakati wa mazoezi nilikuwa nateseka na kuhangaika sana msimu uliopita. Kwa mfano katika kila baada ya vipindi vitatu vya mazoezi basi ilikuwa ni lazima nisimame kwanza kufanya mazoezi, lakini kwa sasa nimeimarika kwa hilo.
"Pia nilikuwa nikifanyiwa matibabu mengi sana wakati wa mazeozi – lakini sasa hivi hapana, naamini itakuwa hivi mpaka nitakapoachana na tasnia hii ya soka.
“Nilienda kwa daktari huko nchini Italy na alinichunguza vitu vingi sana kadiri alivyoweza, na ilinibidi nibadilike kidogo –sasa hivi nimepunguza kula sukari, nyama, ambapo hapo awali nilikuwa nikipenda sana kwa sababu nyama ya Kiargentina ni tamu sana.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video