YANGA SC imetua salama nchini Tunisia na msafara
umeshawasili mjini Sousse ambapo mechi ya marudiano ya hatua ya 16 dhidi ya
Etoile du Sahel itapigwa kesho kutwa jumamosi kuanzia saa 3:00 kwa saa za Tunisia.
Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm anakiongoza kikosi
chake katika mazoezi kuanzia saa 11:00 jioni kwa saa za Tunisia , kwa saa za
Tanzania ni saa 1:00 usiku.
Tunisia wapo nyuma kwa saa mbili ukilinganisha na saa za
Afrika mashariki.
Pluijm amesema kurejea kwa Salum Telela, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
kutaimarisha timu yake katika mchezo huo muhimu.
Hata hivyo imeripotiwa kwamba Yanga walicheleweshwa kwa zaidi ya saa mbili uwanja
wa Ndege baada ya kuwasili mchana na wenyeji wao Etoile walichelewe kufika na kuwapa usafiri, lakini wachezaji, viongozi na wadau wote walioko
huko wako vizuri na wamejiandaa kwa fitina zote.
Etoile waliwapatia basi Yanga lililowasafirisha kutoka mjini Tunis kwenda Sousse kiliometa 140 kutoka mji mkuu Tunis.
Mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Taifa Dar es salaam
takribani majuma mawili yaliyopita, timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Yanga wanahitaji ushindi au
sare ya zaidi ya magoli 2-2 ili
kusonga mbele moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment