Tuesday, April 21, 2015

MBIO za Yanga kutangaza ubingwa mapema zinaanza leo wanapochuana na Stand United katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara inayopigwa uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Yanga inaingia uwanjani bila nahodha wake na baba mwenye nyumba kwenye safu ya ulinzi, Nadir Haroub Ali 'Cannavaro' aliyepata majeruhi mwishoni mwa juma lililopita kwenye mechi ya kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile du sahel ambayo walitoka sare ya 1-1.
Yanga na Etoile zitarudiana wiki mbili zijazo huko Tunisa katika mechi ya pili ya raundi ya 16 bora na mshindi wa jumla atafuzu robo fainali.
"Naikosa mechi kwasababu ya majeruhi, huu ni wakati muhimu kwa klabu yangu, nilitamani kucheza lakini afya hairuhusu. Najua wenzangu watafanya kazi nzuri na wapo katika morali ya juu". Amesema Cannavaro.
Wakati huo huo mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema wanataka kupambana washinde mechi tatu.
“Lengo ni kushinda tatu zote, ili tukienda kupambana na Etoile tayari tunakuwa mabingwa,” alisema Muro.


“Tunajiandaa ili tushinde mechi ya kesho dhidi ya Stand United. Baada ya hapo, ni zamu ya anayefuatia,” alijigamba Muro.

MECHI TANO (5) ZA YANGA ZILIZOBAKI

Yanga v Stand United    uwanja wa Taifa (inachezwa leo)

Ruvu Shootings v Yanga  uwanja wa Taifa 

Yanga v Polisi Moro uwanja wa Taifa

Azam fc v Yanga Uwanja wa Taifa

Ndanda fc v Yanga Uwanja wa Nangwanda Sijaona 

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video