Na Kassim Mtolea
Mwanasoka wa zamani wa Yanga pamoja na timu ya taifa ya Tanzania,Seklojo Johnson Chambua amezungumzia mchezo wa jumamosi kati ya Yanga na Etoile sportivo du Sahel ya Tunisia .
Chambua amesema hakuna ubishi kama timu yake hiyo ya zamani ilizidiwa na wapinzani wao kutoka kaskazini mwa Africa .
"Ukweli wale jamaa walicheza vizuri sana hususani kipindi cha kwanza na mwanzoni mwa kipindi cha pili cha mchezo, naona walivyokuwa wakitengeneza nafasi kitu ambacho Yanga hawakutegemea".
Chambua aliongeza kuwa Yanga walikuwa wanategemea kwamba wageni hao wangelinda goli lakini ikawa tofauti kutokana na waarabu hao kushambulia na hivyo kuitoa Yanga mchezoni.
Akiuzungumzia mchezo wa marejeano ,Chambua amesema mchezo huo utakuwa mgumu lakini kwenye mpira kila kitu kinawezekana.
"Ni jambo la kukaa waalimu na wachezaji kuweka akili zao huko, naamini hakuna kinachoshindikana kwenye mpira wa miguu,japo naamini kuwa itakuwa ngumu kuwafunga waarabu hao kwao"
Chambua amewaomba watanzania kuwaunga mkono wanajangwani kwani wanachokifanya ni kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye anga za kimichezo kimataifa.
0 comments:
Post a Comment