Uongozi wa Yanga umesema kikosi chake kitaweka kambi maalum nje ya nchi
kabla ya kuivaa Etoile Sportive du Sahel (ESS) ya Tunisia katika
michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwezi huu.
Yanga, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara na mabingwa mara tano wa Kombe la Kagame, wamepangwa kucheza dhidi ya ESS katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho mwaka huu wakianzia nyumbani Aprili 17-19 kabla ya kurudiana mjini Tunis, Tunisia Mei 1-3.
Tofauti na ilivyozoeleka kwa timu za Tanzania kuweka kambi maalum zinapokaribia kucheza dhidi ya Simba na Yanga, wanajangwani wameichukulia uzito wa juu mechi dhidi ya ESS kwa kufanya maandalizi makubwa.
Katika mahojiano na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana mchana, Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, alisema kikosi chao kitaweka kambi maalum ughaibuni kabla ya kuikabili timu hiyo kongwe na tajiri.
"Kikosi chetu kimeingia kambini hapa Dar es Salaam leo (jana) asubuhi kwa ajili ya mechi ya kesho (leo) dhidi ya Coastal na ya Jumamosi dhidi ya Mbeya City. Baada ya mechi hizi mbili, tutaweka kambi maalum kwa ajili ya Etoile du Sahel," Muro alisema;
"Tumepanga timu ikae kambini nje ya nchi kabla ya kuikabili Etoile. Tumeomba pia TFF watupe muda wa kufanya maandalizi mazuri kwa kupangua ratiba ya mechi mbili zetu mbili baada ya City ili tujiandae vizuri kwa mechi za kimaifa.
"Ikishindikana kukaa
nje ya mipaka ya Tanzania, hili ikiwa TFF wakikataa kupangua ratiba ya
VPL (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara), tutakaa kambini Bagamoyo au
Zanzibar."
Baada ya kuikabali City Jumamosi, Yanga itacheza dhidi ya ESS na ratiba ya VPL inaonyesha kikosi cha Jangwani kitaikabili jijini Stand United Aprili 22 na Ruvu Shooting Aprili 26 kabla ya kurudiana na ESS Mei 1-3 mjini Tunis.
ESS INATISHA AFRIKA
Étoile ni moja kati ya timu mbili duniani, pamoja na Juventus FC ya Italia, iliyoshinda mataji yote ya ndani yaliyoandaliwa na shirikisho la soka la nchi husika na timu pekee iliyowahi kushinda michuano yote mikubwa ya Afrika kwa ngazi ya klabu.
Baada ya kuikabali City Jumamosi, Yanga itacheza dhidi ya ESS na ratiba ya VPL inaonyesha kikosi cha Jangwani kitaikabili jijini Stand United Aprili 22 na Ruvu Shooting Aprili 26 kabla ya kurudiana na ESS Mei 1-3 mjini Tunis.
ESS INATISHA AFRIKA
Étoile ni moja kati ya timu mbili duniani, pamoja na Juventus FC ya Italia, iliyoshinda mataji yote ya ndani yaliyoandaliwa na shirikisho la soka la nchi husika na timu pekee iliyowahi kushinda michuano yote mikubwa ya Afrika kwa ngazi ya klabu.
Imetwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika mara moja 2007 na kufungwa katika fainali ya michuano hiyo mara mbili 2004 na 2005.
Klabu hiyo ambayo ilimsajili kiungo mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, kwa mali kauli ya dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 500) na kusababisha mgogoro mkubwa ndani ya uongozi ya klabu hiyo ya Msimbazi miaka miwili iliyopita, iliwahi kutwaa Kombe la Shirikisho mara moja 2006.
Imeshinda iliyokuwa michuano ya Kombe la Washindi barani Afrika mara mbili1997 na 2003 na iliyokuwa michuano ya Kombe la CAF mara mbili pia 1995 na 1999 na kufungwa katika fainali ya michuano hiyo mara mbili pia 1996 na 2001.
Imetwaa pia taji la iliyokuwa michuano ya African Super Cup mara mbili 1998 na 2008 na kufungwa katika fainali ya michuano hiyo 2004 na 2007.
INATISHA TUNISIA PIA
Etoile pia imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tunisia mara tisa 1950, 1258, 1963, 1966, 1972, 1986, 1987, 1997 na 2007. Imetwaa pia ubingwa wa Kombe la Rais wa Tunisia mara tisa 1959, 1963, 1974, 1975, 1981, 1983, 1996, 2012 na 2014.
2005 ESS ilishinda Kombe la Ligi Tunisia (FA) na kunyakua taji la Super Cup la Tunisia mara tatu 1973, 1986 na 1987.


0 comments:
Post a Comment