Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Ruvu na Kagera zilitoka suluhu katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu iliyochezwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani Januari 3 mwaka huu.'
KIKOSI cha nyota 20 na viongozi 10 cha Ruvu Shooting Stars kinatarajiwa kusafiri kwenda mjini Shinyanga kesho huku uongozi wa klabu hiyo ya Pwani ukitamba kuigab nyayo za Simba SC kwa kuifunga Kagera Sugar FC katika mechi yao ya mwishoni mwa wiki.
Ruvu Shooting Stars inayonolewa na Mkenya Tom Olaba itakuwa na kibarua kigumu mbele ya kikosi cha Mganda Jackson Mayanja cha Kagera Sugar FC, timu hizo zitakapopambana katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara usukumani Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga Jumamosi.
Masau Bwire, msemaji wa Ruvu Shooting, amesema jijini hapa leo kuwa kikosi chao kitasafiri kesho kwenda Kanda vya Ziwa tayari kuwakabili Kagera ambao Jumatatu walifungwa kibabe 2-`1 dhidi ya Simba SC.
"Kagera Sugar SC ni moja ya timu ngumu inayocheza kitimu, yenye wachezaji wanaojiamini na wenye uchu wa kufumania nyavu, lakini kikosi chetu kimejidhatiti kwa kila idara kuhakikisha tunaibuka na ushindi. Kikubwa waamuzi wachezeshe kwa kufuata Sheria 17 za Soka ili kila timu ipate inachokistahili kutokana na uwezo wake wa kucheza mpira," amesema Bwire.
Aidha, Bwire amesema nyota wao saba wa kikosi cha kwanza hawasafiri na timu leo kwenda mjini Shinyanga kutokana na sababu mbalimbali.
Amewataja wachezaji hao kuwa ni kipa changuo la kwanza, Abdallah Rashid na Salvatoryb Ntebe ambao wana kadi tatu za njano, Juma Mpakala anayeuguliwa na mkewe, Betramu Mwombeki, Stephano Mwasyika, Lambele Jerome na Juma Abdul ambao ni majeruhi.
Ruvu Shooting Stars ambayo haijawahi kuporomoka daraja tangu ipande ligi kuu, iko nafasi ya tano katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 26 baada ya mechi 21, pointi mbili nyuma ya Kagera Sugar FC walioko nafasi ya nne baada ya mechi 21 pia.

.jpg)
0 comments:
Post a Comment