Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WINGU zito limetanda mjini Shinyanga kuelekea katika mechi ya ligi kuu baina ya wenyeji Stand United dhidi ya Mtibwa Sugar inayotarajiwa kupigwa jioni ya leo uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Jana mvua kubwa ilinyesha na kuharibu mandhari ya uwanja wa Kambarage na kusababisha mechi ya Kagera na Simba kuahirishwa hadi kesho jumatatu saa 10:00 jioni.
Hata hivyo kulizuka mgongano mkali wa mawazo ambapo Simba hawakuridhishwa na maamuzi ya kuahirisha mechi wakidai uwanja ulikuwa safiu kuchezewa.
Hali ya hewa mjini Shinya muda huu
Hali ya hewa mjini Shinya muda huu
Ni kweli mechi ingechezwa kama wasimamizi wa uwanja wangekubali ushauri wa kutumia magodoro kufyonza maji yaliyotuama maeneo ya magoli yote.
Licha ya magodoro kusemekama kuwepo uwanjani hapo, wasimamizi walishikilia uamuzi wa kuahirishwa mechi.
Sababu kubwa inayotajwa kusababisha kuahirishwa mechi hiyo ni kukosa mapata kwani mashabiki wengi walichelewa kufika uwanjani kwa hofu ya mvua.
Hata hivyo bado hali ya shinyanga haiko katika uhakika wa kutonyesha mvua, kuna mawingu mazito yametanda mji mzima na kuna kila dalili ya mvua kunyesha kama jana.
Kama itanyesha, maana yake kuna uwezekano wa mechi kutochezwa, lakini kwasababu mechi yenyewe haina uzito, tunaweza kushuhudia ikilazimishwa kucheza hata kwa kufyonza maji kwa magodoro ili kupisha mechi ya kesho.
Kama itaahirishwa manaana yake itachezwa jumanne na itakuwa imaharibu kabisa ratiba ya ligi kuu iliyopangulia mara nyingi.
Mechi nyingine inapigwa leo mjini Tanga ambapo wenyeji Mgambo JKT wanachuana na Polisi Morogoro.




0 comments:
Post a Comment