AMISSI Tambwe mfungaji wa magoli manne katika ushindi wa 8-0 waliopata Yanga dhidi ya Coastal Union jumatano ya wiki hii amekiri kuwa matatizo aliyokuwa nayo Simba yalimfanya kiwango chake cha kufunga magoli kishuke.
Akiongea na mtandao huu, Tambwe amesema anashukuru sasa matatizo yanaisha polepole na ameanza kufunga.
Aidha mshambuliaji huyo raia wa Burundi amesema anaweza kutetea kiatu chake dhahabu kwani sasa anazidiwa magoli manne tu na kinara Simon Msuva, mchezaji mwenzake wa Yanga, huku akizidiwa moja tu na watu wanaoshika nafasi ya pili, Didier Kavumbagu (Azam fc) na Rashind Mandawa (Kagera Sugar) wenye magoli 10.
Pia Tambwe mfungaji wa magoli 19 msimu uliopita amezungumzia mechi ya leo baina ya Yanga na Mbeya City inayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Tambwe (kulia) akishangilia goli na Simon Msuva
Tumejiandaa vizuri, tunakimbizana na Azam, kwa hiyo haturuhusiwi kupoteza mchezo wa leo. Najiamini timu yetu iko vizuri na leo tutafanya vizuri".
Kuhusu kutetea kiatu chake cha dhahabu, Tambe mtaalamu wa magoli ya kichwa amesema, "Lazima mshambuliaji uwe unataka kuwa juu ya wengine, kwahiyo inawezekana nikatetea kiatu changu kwa sasa, nilikuwa nyuma sana na sahizi anayeongoza kufunga ananizidi magoli manne tu"
KWANINI ALIPOKUWA SIMBA MSIMU HUU ALIKUWA NA UKAME WA MAGOLI?
Tambwe anasema: "Mpira upo kichwani, ukishakuwa na matatizo kichwani huwezi kucheza mpira, nilipokuwa Simba nilikuwa na matatizo, lakini yanaisha pole pole na nashukuru nafanya vizuri
"Nawaambia wana Yanga tutafanya vizuri na kuhakikisha timu inakuwa bingwa"
"Kocha Hans van der Pluijm naipata vizuri fundisha yake, ni kocha mzuri"


0 comments:
Post a Comment