YANGA SC inashuka leo jioni uwanja wa Taifa, Dar es salaam kukabiliana na Wagonga nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc katika mechi ngumu ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Hii ni mara ya nne (4) City zinakutana katika misimu miwili ambayo Mbeya City imeshiriki ligi kuu.
Mechi ya kwanza msimu uliopita timu hizo zilitoka sare ya 1-1 uwanja wa Sokoine kabla ya Yanga kuifunga City 1-0 uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Msimu huu mechi ya kwanza Yanga walishinda 3-1 uwanja wa Sokoine na leo zinakutana tena uwanja wa kisasa wa Taifa, Dar es salaam.
Yanga ndio vinara wa ligi kuu wakiwa na pointi 43 kileleni baada ya kucheza mechi 20, wakifuatiwa na Azam fc waliotoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar jana na kufikisha pointi 38.
Kuelekea katika mechi hiyo, Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema haya:
"Kwa upande wetu tumejiandaa vizuri na tunasema kila mchezo kwetu ni fainali, Mbeya City ni timu nzuri ila tu kwetu sisi kila mchezo kwetu ni fainali na tumemaliza mazoezi leo (jana). Wachezaji wana hamu ili tuweze kushinda na kuendelea kuongoza ligi
"Kutokana na kwamba ukiweza kupoteza mchezo mmoja unampa mwenzako faida ya kukusogelea, kwetu sisi tumeona kila mchezo utakuwa fainali na kila mchezo lazima tushinde ili kusogelea ubingwa kwasababu ligi ya mwaka huu ni ngumu, timu ya chini ikiweza kushinda mechi moja anaweza kukaa nafasi ya tano mpaka ya nne, kila mchezo tunahitaji kushinda" . Amesema Cannavaro.


0 comments:
Post a Comment