Wednesday, April 15, 2015

Siku moja baada ya bodi ya ligi kuzilima faini timu zilizokataa kuingia katika vyumba vya kuvalia nguo katika uwanja wa ccm kambarage mkoani shinyanga, bodi hiyo imetuma wakaguzi kuchunguza vyumba hivyo.

Kaimu mkurugenzi wa bodi ya ligi Fatma Abdallah amesema baada ya kuona tatizo hilo likijirudia mara kwa mara katika uwanja huo, wameamua kumtuma mkaguzi mkoani humo kubaini tatizo lililopo katika vyumba hivyo.

Fatma amesema uamuzi huo umekuja kutokana na tatizo hilo kujirudia huku ripoti ya msimamizi wa michezo hiyo ikionesha kuwa vyumba hivyo havina tatizo.

Jana bodi ya ligi ilitoa taarifa ya kuzipiga faini timu za Simba na Mtibwa Sugar kwa kutoingia vyumbani huku miezi ya nyuma timu nyingine ikiwemo Yanga na Mbeya City zimeshawahi kumbana na adhabu hiyo.

Fatma ameongeza kuwa endapo itagundulika kwamba vyumba hivyo vina matatizo basi timu zote zilizopigwa faini kutokana na kutoingia katika vyumba hivyo watafutiwa faini hizo na kurudishiwa fedha zao.

Katika hatua nyingine Fatma amesema kutokana na hali ya ushindani iliyopo hivi sasa katika ligi kuu hususani timu zitakazoshuka daraja, bodi hiyo imeanza mchakato wa kuhakikisha wanadhibiti upangaji wa matokeo.

 kaimu mkurugenzi wa bodi ya ligi amesema kile walichokifanya wakati wa ligi daraja la kwanza ndicho watakachofanya kwenye ligi kuu.

Msimu uliopita wakati ligi daraja la kwanza inaelekea ukingoni bodi hiyo iliweka utaratibu wa kuwatuma wafuatiliaji wa michezo hiyo wasiotambulika kwa ajili ya kusaidia kubaini udanganyifu wowote.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video