MSHAMBULIAJI wa Stand United, Abasirim Chidiebele amefunga goli lake la tisa (9) msimu huu timu yake ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya Maafande wa JKT Ruvu katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyopigwa jioni ya leo uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Goli la JKT Ruvu Stars limefungwa na Samuel Kamuntu.
Taarifa zinaeleza kuwa maafande wa JKT Ruvu waligoma kuingia vyumbani na kukaguliwa kwenye gari lao.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa mashindao wa TFF, Boniface Wambura alikuwepo uwanjani na tunasubiri taarifa yake.
Vyumba vya kubadilishia nguo uwanja wa Kambarage vinalalamikiwa kwa ubovu na timu kadhaa hazikuingia mechi zilizopita ikiwemo Simba na Ruvu Shootings.


0 comments:
Post a Comment