Cannavaro alifunga goli mechi iliyopita Yanga wakishinda 3-1 dhidi ya Mbeya City uwanja wa Taifa
YANGA SC kesho jioni itachuana na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 ya kombe la shirikisho uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub Ali 'Cannavaro' amewaomba watanzania kuwaombea dua njema na wale wataofika uwanjani washangilie kwa nguvu ndani ya dakika zote 90'.
Cannavaro amesema: "Kila mchezaji ana hamu ya kucheza mchezo wa kesho na kila atayepata nafasi ya kucheza ataonesha kiwango. Mungu akitujaalia tutapata ushindi".
"Sisi kwa upande wetu tutashambulia sana, tumejiandaa kupata magoli mengi kwasababu Waarabu siku zote wakija kucheza hawachezi vile unavyotarajia".
"Wanapoteza sana muda, wanataka kumiliki mpira, lakini sisi tunalijua hilo na tunajiandaa kwa ajili ya kuwashambulia ili tupate magoli mengi ambayo yatatusaidia mchezo wa marudiano".


0 comments:
Post a Comment