Monday, April 13, 2015


SIMBA SC imerejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City fc ikitokea kanda ya ziwa ilipocheza mechi na Kagera Sugar ikishinda 2-1 na kushiriki shughuli za kijamii Rorya- Mara na Mwanza.

Mbeya City fc na Simba zitapepetana aprili 18 mwaka huu uwanja wa Sokoine Mbeya.

Watani zao wa jadi , Young Africans jana walishinda 3-1 dhidi ya Mbeya City fc na kuendelea kujikita kileleni mwa ligi kuu wakikusanya pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 wakifuatiwa na Azam fc waliocheza mechi 20 na kukusanya mzigo wa pointi 38

Kituo cha redio cha E FM kilimtafuta msemaji wa Simba Hajji Sunday Manara na kumhoji habari za Simba na hatimaye kumchokoza kwa kumuuliza matokeo ya Yanga.

Mtangazaji wa kituo hicho, Maulid Kitenge ndiye alifanya mahojiano hayo kwa njia ya Simu ambapo Hajji alikuwa anaangalia mechi ya Manchester United dhidi ya Manchester City.

Hajji ni shabiki wa kutupwa wa Simba na Man United na mahojiano yalienda hivi;


Mtangazaji: Leo hii mmesikia Young Africans wakizidi kujikita kileleni?

Hajji: Nani?

Mtangazaji: Young Africans?

Hajji. Eheeeh!

Mtangazaji:Wamezidi kujikita kileleni baada ya kumnyoa Mbeya City

Hajji: Alaaah! Mimi naangalia United na City hapa,hiyo ndo unaniambia wewe

Mtangazaji: Huna taarifa hizo?

Hajji: Naishughulikia Simba, mimi naishughulikia Simba na United

Mtangazaji: Huna taarifa za Yanga?

Hajji: Yanga inanihusu nini? Kwani lazima uniulize mimi, si umuulize msemaji wao au viongozi wao, kwani hawana?

Mtangazaji: Kasi yao ya ligi huioni? Wao ndio vinara

Hajji: Kasi yao  maana yake nini,sisi tunashughulikia mechi zetu, wewe umeuliza habari za Simba nimekujibu, sasa unaniuliza habari za Yanga zinanihusu nini?

Mtangazaji: sasa kasi yao ninyi haiwatishi?

Hajji: Tunamuogopa nani, angalia huku goli la tatu wewe! la United

Mtangazaji: Kwahiyo wewe huna shughuli kabisa na Young Africans?

Hajji: Nilikuwa naangali jinsi ilivyopigwa na Antonio Valencia, Yanga sina shughuli nao.

Mtangazaji: Unawaambia nini sasa Yanga?


Hajji: Niwaambie nini?, mimi ni kiongozi wa Simba na si kiongozi wa Yanga, unaniuliza ya Yanga inanisaidia nini, mimi kiongozi wa Simba, nalipwa na Simba, sina habari za Yanga, unataka kuniingiza sokomoko bwana kila wakati unaniuliza habari za Yanga.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video