Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
KOCHA bora msimu uliopita, Juma Mwambusi wa Mbeya
City fc amefungwa mechi ya tatu kati ya nne alizokutana na Yanga katika misimu
miwili mfululizo waliyoshiriki ligi kuu Tanzania bara tangu wapande mwaka jana.
Hii inatokana na kipigo cha 3-1 walichopata jana
uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga, huku wakiwa pungufu kwa dakika 37’ za mchezo
kutokana na Themi Ferlix kuoneshwa kadi nyekundu na muamuzi Mathew Akrama baada
ya kumchezea rafu mbaya Salum Telela ambaye baadaye dakika ya 61 alishindwa
kuendelea na mchezo.
Mechi mbili za msimu uliopita, Mbeya City ilitoka
sare ya 1-1 na Yanga uwanja wa nyumbani wa Sokoine kabla ya kufungwa 1-0 uwanja
wa Taifa.
Msimu huu mechi ya kwanza walifungwa 3-1 uwanja wa
Sokoine na jana wamefungwa kipigo kama hicho uwanja wa Taifa.
KOCHA MWAMBUSI ANASEMAJE KUHUSU KIPIGO HICHO?
![]() |
| Juma Mwambusi |
“Bahati mbaya sijasikitika kwa matokeo niliyopata
kwasababu katika matokeo mengi nimekuwa nikifanikiwa, nilikuja uwanja wa Taifa
na kushinda (2-1 dhidi ya Simba januari 28 mwaka huu). Sema ninasikitika tu
kwasababu nimepoteza na nilikuwa nahitaji ushindi, mpira una matokeo matatu,
ninachosema ni kwamba nimepambana. Mpaka tunakwenda mapumziko tulikuwa
tumefungwa magoli 2-1 na tuliporudi kipindi cha pili wakaongeza goli la tatu
dakika za mwanzo”
ANAIZUNGUMZIAJE KADI NYEKUNDU YA THEMI FELIX?
Mwambusi anasema: “Lakini tulichanganywa na kadi
nyekundu ya muamuzi, ilikuwa na matatizo, basi tunakubali kuwa tumefungwa 3-1 na
Yanga na tunajipanga kwenda kupambana na Simba Mbeya”
KUELEKEA MECHI YA SIMBA ANAWAAMBIA NINI MASHABIKI
WA MBEYA CITY FC?
Mwambusi anajibu: “Wapenzi wa Mbeya City ambao
wapo nchi nzima kwanza niwashukuru kwa kutuunga mkono kwa kiasi kikubwa,
ninachosema mechi imeshaisha, tunayasahau na tunaenda kupambana na Simba kuhitaji
pointi tatu pale nyumbani. kwahiyo waje watupokee kwa hamasa kubwa, wachezaji
wamejipanga, watuombee tufike salama katika safari yetu ili tujiandae vizuri”
Mbeya City fc na Simba zitapambana jumamosi aprili
18 uwanja wa Sokoine Mbeya katika mfululizo wa ligi kuu soka Tanzania bara.



0 comments:
Post a Comment