Monday, April 13, 2015


KAGERA Sugar wanaikaribisha Ruvu Shootings katika mechi pekee ya ligi kuu soka Tanzania bara inayopigwa leo jioni uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Awali mechi hiyo ilipangwa kufanyika jumamosi ya wiki iliyopita, lakini iliahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha na uwanja wa kujaa maji.
Kagera walikumbwa na mkasi jumamosi ya pasaka (Aprili 4) mwaka huu ambapo mechi yao dhidi ya Simba iliyotakiwa kupigwa siku hiyo iliahirishwa mpaka jumatatu ya aprili 6 kutokana na uwanja wa Kambarage kujaa maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Shinyanga.
Aprili 5 mwaka huu mechi ya Stand United dhidi ya Mtibwa Sugar ilivunjika dakika ya 33' kutokana na mvua kubwa kunyesha na hatimaye mechi kuchezwa kesho yake asubuhi (aprili 6) kwa dakika 57 zilizosalia na baadaye jioni Siku hiyo Kagera walifungwa 2-1 na Simba.
Jumamosi ya wiki iliyopita (aprili 11) mechi ya Kagera Sugar dhidi ya Ruvu Shooting iliahirishwa na inachezwa leo jumatatu (aprili 13 mwaka huu).
Ni mazingira yale ya Kagera na Simba yamejirudi, je, watafungwa kama ilivyotokea kwa Simba na kurudia rekodi yao au watavunja rekodi hiyo? tusubiri tuone itakuwaje.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video