Sunday, April 19, 2015

Beki wa zamani wa Simba sasa Mbeya City, Juma Nyoso (aliyepaa juu) alikuwa kisiki kwa Simba jana.

WEKUNDU wa Msimbazi Simba tayari wamesharejea Dar es salaam leo na wameingia moja kwa moja kambini kujiandaa na mechi ya jumatano ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mgambo JKT itayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Simba jana ilifungwa mabao 2-0 na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine Mbeya.
Afisa habari wa Simba Hajji Sunday Manara amesema: "Tuko Dar es salaam na wachezaji wako kambini moja kwa moja kambini chuo kikuu cha Dar es salaam kujiandaa na mechi dhidi ya Mgambo JKT jumatano"
"Jana lazima niwe mkweli hatukucheza vizuri na inatokea kwenye mpira wa miguu, hamuwezi kucheza vizuri siku zote, mpira ni mchezo wa makosa sana, ukicheza vibaya na kufanya makosa wenzio wanakuadhibu, jana tuliadhibiwa kutokana na makosa yetu".

KOCHA GORAN KOPUNOVIC ANASEMAJE BAADA YA KIPIGO HICHO?

Kwa niaba ya Kopunovic, Hajji amesema:"Hakuna kitu kingine chochote, hii nazungumza kwa niaba ya kocha wa timu na sio maneno ya porojo, "Mechi na Mgambo tunaingalia kwa jicho pana sana, Simba ametoka kujeruhiwa, Mgambo waje vizuri, inawezekana tukamaliza hasira zetu jumatano, mechi tunaichukulia kwa uzito mkubwa sana"
Simba ipo nafasi ta tatu katika msimamo ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 22.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video