Thursday, April 9, 2015


Msemaji wa Wekundu wa Msimbazi Simba SC, Haji Manara amesema kuwa suala la Yanga kuwafunga Wagosi wa Kaya, Coastal Union 8-0 sio suala la kushangaza kwani sio mara ya kwanza kwa timu za Tanzania kutoa kipigo kama hicho.
Manara alisema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha redio cha EFM ambapo alisema kuwa Simba wameshawahi kutoa kipigo zaidi ya hicho mara baada ya kuimaliza timu ya soka ya Mwadui kwa goli 14, hivyo sio suala la kuipa Yanga sifa zilizopitiliza.
Hata hivyo Manara aliongeza kuwa wao kama Simba wanathamini sana masuala ya kijamii, hivyo wamepanga kwenda kutembelea kituo cha kukuzia vijana kisoka kinachojulikana kama Marsh Academy kilichopo jijini Mwanza ambacho kilikuwa kinamilikiwa na aliyekuwa mkufunzi msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Sylvestre Marsh ambaye amefariki mwishoni mwa mwezi February.
Manara aliendelea kusema kuwa baada ya kufanya ziara hiyo watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Toto African, ambayo pia ni ya humo humo  jijini Mwanza

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video