Thursday, April 9, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Yanga SC imerudia rekodi yake ya kushinda mabao mengi zaidi katika Ligi Kuu ya Bara ilipoitandika 8-0 RTC Kagera (sasa Kagera Sugar FC) huku mshambuliaji wake Edibily Lunyamila akiweka rekodi ambayo haijavunjwa ya kufunga hat-trick mbili katika mechi moja.'

JUMATANO Aprili 8, 2015 ni siku ambayo kwa hakika haitasahaulika katika vichwa vya wapenzi na wanachama wa Coastal Union FC na kocha mkuu wao wa muda, Jamhuri Kihwelo 'Julio'.

Ni siku ambayo mashabiki wa Yanga SC wameibatiza jina la 'Tarehe Coastal Mwezi Tambwe' wakimaanisha siku ambayo Coastal Union FC ilibamizwa mabao 8-0 dhidi ya Yanga SC huku mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe, akifunga mabao manne (mwezi wa nne) peke yake.

Hata hivyo, Yanga SC ni kama imekifunga kikosi B cha mabingwa hao wa 1988 wa Tanzania Bara kwani Wagosi wa Kaya jana walianza na wachezaji watatu tu wenye uhakika wa namba katika kikosi chao cha kwanza cha msimu huu.

Kikosi cha Coastal kilichoanza jana kilikuwa na kipa Bakar Fikirini ambaye jana ilikuwa mechi yake ya tatu msimu huu kupangwa langoni akianzia mechi waliyolala 1-0 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Machi 22, mwaka huu.

Hapakuwa na tatizo kwa mabeki wa pembeni kwani walikuwapo Hamad Juma na Abdallah Mfuko ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakianza katika kikosi cha Wagosi hao wa Kaya, ingawa Juma amekuwa na tatizo la utovu wa nidhamu katika baadhi ya mechi.

Katika safu ya mabaeki wa kati kulikuwa na tatizo kutokana na kutokuwapo kwa Tumba Suedi. Mabeki wa kati ja walikuwa Yusuph Chuma na Bakari Mtama. 

Safu ya kiungo licha ya kuwamo kwa kiungo wa zamani wa Simba SC, Abdulhalim Humoud, ilimkosa kiungo fundi na mchezaji bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya Bara, Joseph Mahundi ambaye haijaelezwa na uongozi wa Coastal sababu zilizomfanya akosekana hata katka benchi la timu hiyo jana.

Safu ya ushambuliaji ya Coastal jana ilikuwa na mawinga Ayoub Yahya na Mkenya Rama Salim pamoja na washambuliaji Rajab Mohamed na Ike Bright.

Lakini, katika safu hiyo, ni Rama tu mwenye uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza cha Coastal Union. Alikuwa wapi Lutimba Yayo? Kwa nini hakuwapo hata benchini jana? Kwa nini kipa Shaaban Kado hakuwapo hata benchini jana?

ITAENDELEAA

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video