Hassan Kessy
UONGOZI wa Simba imetangaza rasmi kumalizana na beki wake mahiri wa kulia, Hassan Ramadhan Kessy baada ya kutokea kutoelewana siku za karibuni na kumfanya nyota huyo ajitoe kwenye kikosi.
Kessy aliviambia vyombo vya habari kabla ya Simba kwenda Shinyanga kucheza na Kagera Sugar kuwa anaidai Simba milioni 5 zilizosalia katika ada yake ya usajili na uongozi haukutimiza ahadi ya kumpangia nyumba.
Kessy alisajiliwa na Simba kutokea Mtibwa Sugar katika dirisha dogo mwezi desemba mwaka jana.
Tayari uongozi wa Simba umekutana na mchezaji na kumpatia fedha za kupanga nyumba, huku fedha zake za usajili utaratibu ukiendelea kufanyika.
Msemaji wa Simba, Hajji Manara amekaririwa jioni hii na kituo cha redio cha E FM akisema; "Suala la Kessy hatima imeshafanyika, yeye kama binadamu kwa maana alikuwa na madai yake, klabu imeyatimiza madai yake, lakini kubwa ameiomba radhi klabu"
Hakuna taasisi isiyodai wala kudaiwa, kwahiyo yeye kama binadamu, labda umri wake ni mdogo, aliongea kwenye vyombo vya habari bila kufuata utaratibu kwasababu mkataba wake unambana kuzungumza masuala yoyote au kuzungumza jambo lolote bila kibali cha klabu"
Hajji ameongeza, " Tumelimaliza katika misingi ya kibinadamu na kesho ataanza mazoezi baada ya kuonana na uongozi. Kubwa ni kwamba jambo hili mjadala wake umeshafungwa na ataendelea kuitumikia klabu".
"Tumerejea jijini Dar es salaam, tunajiandaa kuekelekea Mbeya kwenye mchezo wetu na Mbeya City tarehe 18 mwezi huu, nadhani ndio maandalizi yetu hivi sasa".


0 comments:
Post a Comment