Sunday, April 12, 2015


BAO pekee la Mnigeria, Abasirim Chidiebele limewapa Stand United pointi tatu katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Polisi Morogoro iliyopigwa  uwanja wa CCM Kambarage jioni ya leo.
Stand wameshinda mechi ya pili mfufulizo baada ya mwanzoni mwa wiki hii walishinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi iliyochezwa siku mbili.
Awali ilivunjika siku ya jumapili dakika ya 33'  Stand wakiongoza kwa bao moja lililofungwa na Haruna Chanongo na akachezwa jumatatu asubuhi kwa dakika 57' zilizosalia.
Chidiebele leo amefikisha bao lake la nane (8) msimu huu.
Kwa matokeo ya leo, Stand United wanapanda kutoka nafasi ya 11 mpaka nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi kuu.
Ligi kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja, Kagera Sugar watachuana na Ruvu Shootings uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video