KOCHA mkuu wa Kagera Sugar, Mganda Jackson Mayanja ametamba kuichapa Simba katika mechi yao ya ligi kuu itakayochezwa kesho jioni uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga kuanzia saa 10:00.
Mechi hiyo ilitakiwa kuchezwa jana lakini iliahirishwa mpaka kesho kutokana na uwanja wa Kambarage kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa mjini Shinyanga.
Akizungumza na mtandao huu mjini Shinyanga, Mayanja amesema anawahurumia Simba kama vijana wake watafanya kile alichowafundisha.
"Mimi sihofii mtu yoyote,naihofia tu timu yangu, kama watafanya kilekile nilichowafundisha kwenye mazoezi watawaua Simba. Kama hawatafanya vile nilivyowafundisha hapo ndipo nitaanza kupata hofu, lakini sitishiki eti kwasababu hii ni Simba au Yanga". Amesema Mayanja na kuongeza,"Nawaogopa tu vijana wa Kagera kama wanafanya kile tunachotaka, wanaweza kuiua timu yoyote kama waamuzi wanafuata kanuni, hicho ndicho naamini
Falsafa yangu ni kwamba napoteza mechi kwa staili nashinda kwa staili, sitaki kushinda bila staili. Unaona timu inashinda 3-0, 2-1, lakini huoni mpira, hiyo haina maana"
Hata hivyo Mayanja hatakaa kwenye benchi kwasababu alioneshwa kadi nyekundu katika mechi ya katikati mwa wiki ambayo timu yake ilishindi 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.
Desemba 26 mwaka jana uwanja wa Taifa, Atupele Green aliifungia Kagera bao moja katika ushindi wa 1-0 waliovuna dhidi ya Simba.

.jpg)
0 comments:
Post a Comment