Sunday, April 5, 2015



MAPEMA leo asubuhi mtandao huu uliripoti hatihati ya pambano la Stand United na Mtibwa Sugar kufanyika kutokana na hali ya hewa kutanda wingu zito lililonesha dalili ya mvua kubwa kunyesha.
Lakini mchana kutwa mvua haikunyesha na jua liliwaka kwa kiasi fulani, lakini kulikuwa na wingu.
Baadaye saa 10:30 jioni pambano likaanza uwanja wa CCM Kambarage  na ghafla manyunyu yakaanza kunyesha na muda mfupi mvua kubwa ikaanza kupigwa.
Muamuzi wa kati Ahamad Simba alichezesha pambano hilo kwa dakika 33 tu na tayari kufikia muda huo Stand United walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa dakika ya 12' na Haruna Chanongo baada ya kazi nzuri ya Mnigeria Abasarim Chidiebele aliyewapiga chenga mabeki wa Mtibwa eneo la mita sita kutoka golini.
Mechi hiyo itarudiwa kesho saa mbili kwa dakika 57 zilizosalia.
Jana mechi ya Kagera Sugar na Simba SC iliahirishwa  kutokana na uwanja wa Kambarage kujaa maji.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video