KOCHA msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa 'Master' amesema klabu hiyo imechelewa kwenda Zimbabwe kuikabili FC Platinum kwa lengo la kukwepa gharama.
Yanga inaendelea kufanya mazoezi katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume, Ilala, Dar es salaam ikiwa na mtaji wa mabao 5-1 waliyopata kwenye mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Taifa Dar es salaam machi 15 mwaka huu.
Ili kusonga mbele, Yanga inahitaji sare tu au kipigo kizichozidi magoli 3-0.
Wakifungwa 4-0 watatupwa nje kwa goli la ugenini walilofunga Platinum kwani wastani utakuwa 5-5.
"Tumechelewa kwenda Zimbabwe kwasababu ya kukwepa gharama, ukienda mapema unatumia fedha nyingi. Tumefanyia utafiti hali ya hewa ya Zimbabwe na kubaini haina tofauti na Tanzania, tutakwenda Ijumaa, tutafanya mazoezi siku hiyo jioni tayari kwa mechi ya kesho yake". Amesema Mkwasa.
Naye nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema wanajua changamoto iliyopo mbele yao, lakini wako fiti kuwatupa nje Wazimbabwe.
"Wachezaji wako fiti kwa kila kitu, tutapambana sana, nilishacheza Zimbabwe, hali ya hewa inafanana na huku japokuwa sisi ni joto sana". Amesema Cannavaro.
0 comments:
Post a Comment