Saturday, April 18, 2015

Bondia Thomas Mashali

Na Kassim Mtolea, Mwanza

SIKU moja baada ya bondia Mada Maugo kutangaza kuwa Thomas Mashali yupo huru,  mambo bado kwa PST.
Katibu mkuu wa shirikisho la masumbwi hapa Tanzania (PST), Anthony Luta amesema adhabu ya Mashali ipo pale pale na hakuna mabadiliko yoyote.

"Tunachojua kama shirikisho Thomas anatumikia adhabu yake ya miaka miwili kama tulivyoitoa kwa utovu wa nidhamu,hicho unachoniambia hata mimi nakisikia kinazungumzwa tu'".

Luta amesema kuna baadhi ya vyama vya masumbwi ambavyo vimechukua suala hilo kama faida yao ili nao wafufuke baada ya kukosa mvuto kwenye mchezo huo.

"Unajua kuna vyama ambavyo vimepotea katika mchezo huu lakini kwa sasa wanaona hii kama turufu kwao kufufuka,si unajua ukitaka kumjua mume mwenzio muache mkeo baada ya sisi kumfungia wao wamemchukua".

MPENJA BLOG ilimbana katibu huyo akitaje chama ambacho kimemchukua Mashali, katibu huyo alikitaja chama hicho kuwa ni chama cha ngumi za kulipwa nchini(TPBC).
Amesema kwamba wana amini bondia huyo kamwe hawezi kupanda ulingoni  mpaka amalize adhabu yake au wamfungulie.
"Mashali hawezi panda ulingoni kwa sasa mpaka tuamue sisi kumaliza adhabu yake maana hata mapromota wanamtafuta na polisi sasa huyu mtu atachezaje?"aliuliza Luta.

Bondia Thomas Mashali anahusishwa na tabia za kusaini mikataba na mapromota au vyama vya ngumi na baadaye kuingia mitini bila kupanda ulingoni kama alivyofanya mwezi machi mwaka huu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video