Sunday, April 19, 2015

MAAFANDE wa Tanzania Prisons 'Wajelajela' wametoka sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Mvua inayoendelea kunyesha jijini Mbeya imeharibu  uhondo wa pambano hilo, lakini kutokana na uwanja wa Sokoine kuwa katika hali nzuri ya kutotuamisha maji mechi imechezwa kwa dakika zote 90'.
Mtibwa Sugar walianza kuandika goli la kuongoza katika dakika ya ya 40' kupitia kwa  Musa Hassan Mgosi aliyefunga  akimalizia mpira uliogonga mwamba baada ya yeye mwenye kupiga kichwa kumalizia kona iliyochongwa na Said Mkopi kutoka winga ya kushoto.

Dakika ya 75’ Meshack Suleiman aliangushwa na muamuzi kuamuru mkwaju wa penalti ambapo ulikwamishwa kimiani na Lugano Mwangama.
Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar wamefikisha pointi 28, wakati Prisons wamefikisha 22, lakini bado wanaendelea kushika nafasi ya pili mkiani.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video