Zikiwa zimebaki siku chache kuelekea pambano la karne la ngumi kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao litakalopigwa katika ukumbi wa MGM Grand huko Las Vegas wikiendi hii,bondia mfilipino Pacquiao amewahakikishia ushindi mashabiki wake.
Akiongea hapo jana katika hoteli ya Mandalay Bay huko Las Vegas Manny amesema kuwa anaenda kuwahakikishia mashabiki wake kile alichowaahidi.
"Siwezi kusema Mayweather ni mpinzani mkali kwangu.Ninajiamini kuliko mapambano yangu mengine niliyowahi kupigana .Sasa anaenda kupoteza pambano kwa mara ya kwanza" alisema Manny.
"Ninajua ninaenda ulingoni kushinda hili pambano. kwa hiyo tulieni ,mimi ndie ninayeenda kupigana. " aliongeza Pacquiao.
Mpaka sasa Pacquiao amepigana mapambano 57 na kushinda 38 kwa KO huku mpinzani wake Floyd Mayweather akiwa ameingia ulingoni mara 47 na kushinda mapambano 26 kwa KO.


0 comments:
Post a Comment