Mexime alikuwa sehemu ya mafanikio ya Mtibwa Sugar FC ilipotwaa ubingwa mara mbili mfululizo 1999 na katika mwaka wa mabadiliko ya karne.'
UONGOZI wa Mtibwa Sugar FC umesema hauna mpango wa kuachana na kocha mkuu wake, mzawa Mecky Mexime, kwa kuwa bado una imani naye.
Msemaji wa Mtibwa Sugar FC, Thobias Kifaru, ameuambia mtandao huu leo kwa simu kuwa bado wana imani kubwa na Mexime, licha ya kufanya vibaya katika miaka yake mitatu mfululizo ndani ya mabingwa hao wa 1999 na 2000 wa Tanzania Bara.
"Mecky ni kijana wetu, tuna imani naye na anafanya kazi nzuri ingawa msimu huu umekuwa mgumu kwetu, amesema Kifaru.
Mtibwa kwa sasa iko nafasi ya saba katika msimamo wa VPL na haina uhakika wa kuwamo katika ligi hiyo msimu ujao
0 comments:
Post a Comment