Wednesday, April 29, 2015

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho, amekubaliana na kauli ya Nguli wa zamani wa Arsenal Thiery Henry (TT), kuwa endapo Arsenal itafanya usajili wa wachezaji wanne wa kiwango cha dunia, basi wanaweza kuirudia rekodi yao ya mwaka 2004 ambapo walimaliza ligi bila ya kufungwa.
Jumatatu ya wiki hii, Henry alisema kuwa Wenger anahitaji kuongeza wachezaji wanne tu wenye ubora wa hali ya juu kabisa ili kuweza kupambana na Chelsea katika kutafuta taji la ligi kuu msimu ujao. 
"Arsenal wana kikosi cha kutisha sana. Lakini wanahitaji kuongeza wachezaji wanne tu, wakifanya hivyo nakuhakikishia kuwa watamaliza msimu bila ya kufungwa tena kama ilivyokuwa msimu wa 2003/2004.
Mourinho pia kwa upande wake aliongeza kuwa klabu kama Manchester United, Liverpool na Manchester City nao watafanya usajili wa nguvu katika dirisha la usajili litakaloanza mwishoni mwa msimu huu kutokana na matokeo yasiyoridhisha walioyapata msimu huu.
Mourinho: "Manchester United wana kikosi ambacho ninaweza kusema ni bora kabisa, ukizingatia wana mchezaji ambaye alivunja rekodi ya usajili ligi kuu nchini Uingereza, Angel Di Maria, ambaye hata hivyo pia hana nafasi katika kikosi hicho.
"Hii inaonesha jinsi gani wana kikosi bora . Ni klabu ambayo ambayo 'Financial Fair' haina nafasi kubwa sana na wanaonekana bado wana nafasi kubwa sana ya kuboresha kikosi katika dirisha la usaji litakaloanza mwishoni mwa msimu.
"City nao wamefanya vizuri sana, kushinda mataji mawili ndani ya miaka mitatu na bado pia wanaonekana wana ni ya kuboresha kikosi chao mwishoni mwa msimu pia, sawa sawa kwa upande wa Liverpool.
"Msimu ujao utakuwa ni mgumu sana kuliko huu unaoelekea mwishoni. Ni ngumu sana kwa timu kutawala kwa kipindi kirefu. Hapa sio Ujerumani ambapo Bayern Munich wanatawala. Sio Uswizi ambapo kuna FC Basel. Na wala sio Scotland ambapo Celtic ndiyo vidume. Ni ngumu sana hapa kwa kweli."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video