Tuesday, April 7, 2015

AZAM FC na Mbeya City zimekutana mara tatu katika mechi za ligi kuu soka Tanzania bara tangu City wapande ligi kuu mwaka jana.
Msimu wa kwanza wa City mwaka jana, mechi ya kwanza walicheza Azam Complex na kutoka sare ya 3-3.
Siku hiyo Watanzania walimtambua rasmi straika mkali wa Mbeya City, Mwegane Yeya kwa kufunga 'Hat-trick' kwa magoli makali ya kichwa.
Mechi ya mzunguko wa pili Mbeya, Azam wakashinda 2-1 na ndio mechi iliyowapa ubingwa rasmi.
Msimu huu, Azam walianzia Mbeya na wakashinda 1-0, goli pekee la Aggrey Morris kwa shuti la mpira wa adhabu ndogo.
Je, kesho Mbeya City wataendeleza rekodi ya kufungwa na Azam fc?

WAO WANASEMAJE?
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Juma Mwambusi amesema wanatambua ugumu wa Azam fc, mabingwa watetezi, lakini katika mpira wanaamini kwamba lolote linaweza kutokea.
"Tumetoka kupata sare ya 1-1 na Ndanda fc, tukishinda dhidi ya Azam itatuweka nafasi nzuri zaidi katika msimamo wa ligi. Tutapambana kwa nguvu zote kuhakikisha tunashinda na kuondoa mtazamo kuwa City ni kibonde kwa Azam fc" Amesema Mwambusi.
George Best Nsimbe, kocha wa Azam fc anasema: "Tuna mechi 4 ndani ya siku 11 ikiwemo ya kesho na Mbeya City fc, hakika tunatakiwa kushinda kama tunahitaji ubingwa, tuko tayari kwa mechi na wachezaji wanafahamu cha kufanya".

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video