YANGA SC ni timu pekee iliyofunga magoli mengi zaidi msimu huu (28) na kufungwa machache (11) wakifuatiwa na Azam fc waliofunga magoli 25 na kufungwa 12.
Pia ni timu ya pili kuwa na mechi nyingi mkononi (mechi 7) wakiwa nyuma ya Azam fc wenye mechi 8 mkononi.
Yanga ni timu inayoongoza ligi kwa pointi 40 ikifuatiwa na Azam fc wenye pointi 36.
Yanga ni timu yenye mshambuliaji mwenye mabao mengi zaidi yaani kinara, Saimon Msuva (magoli 11).
Cha zaidi ndio timu pekee iliyosalia michuano ya kimataifa na itakabiliana na Etoile du sahel katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya kombe la shirikisho baada ya kufanikiwa kuwatoa BDF XI raundi ya awali kwa jumla ya magoli 3-2 na FC Platimum raundi ya kwanza kwa jumla ya magoli 5-2.
Rekodi mbaya katika michuano hiyo ni kwamba Yanga wameshinda mechi za nyumbani tu na kupoteza zote mbili za ugenini.
Pia ni timu inayoongoza kubeba kombe la ligi kuu, mara 24 wakifuatiwa na Simba mara 18.
Wakiwa katika mazingira mazuri namna hiyo, kesho wanachuana na Coastal Union katika mechi ya ligi kuu itakayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Mechi ya kwanza walishinda 1-0 uwanja wa Mkwakwani Tanga, bao la Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema: " Kama unataka kuwa bingwa lazima ushinde kila mechi, Coastal ni timu nzuri, tutaendelea kuwa na nidhamu ya mchezo na tutashinda kesho".
Kesho watashinda au itakuwaje? tusubiri.....


0 comments:
Post a Comment