SIMBA SC wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa
ligi kuu wakijikusanyia pointi 35 baada ya kucheza mechi 21 sawa na Azam wenye
pointi 39 nafasi ya pili.
Tofauti ya Simba na Azam ni kwamba Wanalambalamba
wameshinda mechi nyingi zaidi ukilinganisha na Mnyama.
Azam wameshinda 10, sare 9 na kufungwa 2.
Wamefunga magoli 27 na kufungwa 14, tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni
13.
Simba wao wameshinda mechi 9, sare 8 na kufungwa
4. Wamefungwa magoli 27 na kufungwa 15, tofauti ya magoli ni 12.
Mbeya City fc wapo nafasi ya 10 kwa pointi 25
baada ya kucheza mechi 22. Wameshinda mechi 5, sare 10 na kufungwa 7. Wamefunga
magoli 17 na kufungwa 21, tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni -4.
Kwa jinsi msimamo ulivyo, kati ya Mbeya City na
Simba, Mnyama hawezi kushuka daraja, lakini Mbeya City kama hawakazi lolote
linaweza kutokea.
Timu tatu tu, Yanga, Azam, Simba ziko salama,
lakini nyingine zote zinaweza kushuka daraja.
Timu ya 12 katika msimamo (JKT Ruvu) ina pointi 24
ikitofautiana na Mgambo JKT iliyopo nafasi ya tano kwa pointi 4 tu kwasababu
Mgambo wana 28.
Kutokana na Azam kuteleza mechi tatu wakivuna
pointi tatu tu, wamekaribiana sana na Simba, kitu kilichompa nguvu kocha mkuu
wa Wanamsimbazi, Goran Kopunovic nguvu ya kuisaka nafasi ya pili.
Kwa miaka miwili Simba hawajapanda ndege kwenda
kucheza mechi za kimataifa. Kumbuka kwa mara ya mwisho kutwaa ubingwa ni msiamu
wa 2011/2012. Msimu uliofuata (2012/2013) walishika nafasi ya tatu Azam
wakishika nafasi ya pili, Yanga wakitwaa ubingwa.
Msimu wa 2013/2013 Simba walishika nafasi ya nne,
ya tatu ikashikwa na Mbeya City, ya pili Yanga na bingwa akawa Azam fc.
Bila shaka wanataka kufuta makosa baada ya Azam
kuwapa mwanya.
Kwa kuanza harakati zao wanachuana na Mbeya City
uwanja wa Sokoine keshokutwa katika mechi ya ligi kuu.
Kocha Kopunovic amesema: “Sasa kuna mwanga mbele
yetu, kama tutashinda mechi 5 zilizosalia kuanzia ya Mbeya City tunaweza kukaa
nafasi nzuri kutegemeana na matokeo ya Azam. Imekuwa safari ndefu, lakini
tumekuwa tukiimarika kadri siku zinavyokwenda”.
“Mbeya City ni timu nzuri, wametoka kufungwa na
Yanga ingawa walicheza soka zuri, tumekuwa na muda kidogo wa kujiandaa toka
tulipocheza na Kagera, tuko tayari kwa ajili ya mechi, tuwaambia mashabiki
wangu, mashabiki wa Simba, tuwape moyo vijana wetu”.
Kwa upande wa kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi
amesema: “Tunamshukuru Mungu tunaendelea vizuri na maandalizi yetu kuisubiri
Simba jumamosi, utakuwa mchezo mgumu, lakini siku zote sisi tunajiandaa kwa
mechi 26 za ligi. Tumeacha pointi tatu Dar es salaam, lakini kumbuka tulichukua
3 kutoka kwa Simba, tunajitahidi kutumia vizuri faidi ya nyumbani na tunaamini
tutashinda”.
Kama Mbeya City watashinda itakuwa jambo zuri
kwako katika harakati za kukwepa kushuka daraja, lakini Simba wakishinda
watazidi kuwachanganya Azam katika nafasi ya pili.
Azam wao watacheza dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa
Azam Complex.


0 comments:
Post a Comment