MTANDAO wa michezo wa Sky SPORTS umeripoti kwamba Diego Maradona amemshambulia na kumfananisha na 'Shetani' kocha wa Manchester United, Louis van Gaal kwa namna anavyomtumia Radamel Falcao.
Mcolombia huyo ambaye amekaa benchi katika mechi tano zilizopita amefunga magoli manne (4) tangu asajiliwe kwa mkopo wa mrefu kutoka Monaco.
Van Gaal ana nafasi ya kumfanya Falcao apewe mkataba wa kudumu katika kikosi chake utakaogharimu paundi milioni 43 majira ya kiangazi mwaka huu, lakini Mshindi huyo wa kombe la Dunia , Maradona amesisitiza kuwa hajampa Falcao nafasi ya kuonesha thamani yake Old Trafford.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mechi ya hisani itayopigwa Bogota, Colombia, Maradano amekaririwa akisema: "Van Gaal si mtu mzuri. Van Gaal anakaribia kuwa shetani kuliko kitu kingine"
Maradano ambaye aliitazama United ikipoteza nyumbani dhidi ya Liverpool msimu uliopita anashawishika kuamini kuwa Falcao ameathiriwa sana na majeruhi kubwa ya goti aliyopata msimu uliopita, hivyo imemzuia kuonyesha uwezo wake na ameshindwa kuzoea kwa haraka mazingira ya England.


0 comments:
Post a Comment