KOCHA wa Yanga Hans van der Pluijm amesema kipigo cha bao 8-0, walichokitoa juzi dhidi ya Coastal Union kimemshangaza kwani hajawahi kupata matokeo kama hayo tangu aanze kufundisha soka kwenye nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Ghana na Saudi Arabia.
Pluijm amesema timu yake ilistaili ushindi katika mchezo huo kutokana na kuonyesha mchezo mzuri na kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa licha ya makosa madogo madogo waliyokuwa nayo wapinzani wao Coastal.
“Haya ni maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu wa michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile du Sahel, tunakikosi imara kinachoweza kufunga idadi kubwa ya mabao kama ilivyokua juzi tulipowafunga Coastal Union imekuwa ni kama mshangao kwangu kwa sababu huko nyuma tulikuwa tunapata ushindi kwa tabu lakini juzi ilikuwa tofauti,”amesema Pluijm.
Aprili 18 Yanga kama wawakilishi pekee kwenye michuano ya 16 watawakaribisha mabingwa wa zamani wa Afrika Etole du Sahel ya Tunisia, katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya 16 bora na endapo itaitoa timu hiyo itaingia hatua ya makundi.

0 comments:
Post a Comment